Seneta wa Kaunti ya Nyamira Kennedy Mong’are Okong’o ameanzisha mradi wa upanzi wa miti katika kaunti hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea katika eneo la Tong’a Nyamaiya Seneta huyo alisema kuwa anataka kuona kaunti hiyo ikiwa na misitu 45% kutoka 35% katika kaunti hiyo ili kuona amefikia mahitaji ya mazingira.

Seneta huyo alikabidhi eneo la Bosiango na  Nyambaria miti 6,000 kila moja ya maeneo hayo mawili na kusema anahitaji miti ipandwe kwa shule,hospitali, soko na katika  makanisa.

Shule 15 za msingi sitanufaika na mradi huo wa upanzi wa miti ikiwamo shule ya Kura,Rangenyo,Marara na zingine sikiwa mojawapo ya zile zitanufaika huku shule 5 za upili pia zikinufaika na mradi huo ikiwamo shule ya Rateti ,Gekomoni na zikingine zikinufaika zaidi.

“Nahitaji kaunti yetu iwe na mazingira mema wageni wakitembea kwa kaunti hii yetu wapate mazingira yetu yametuzwa vilivyo,”alidokeza Okong’o.

Wakati huo huo Seneta huyo ameomba Gavana na wananchi wa kaunti hiyo kuunga mkono mradi huo ambao unajulikana kama Mong’are foundation.

Mradi huo umekuwa ukisubiriwa kwa Kaunti hiyo baada ya Seneta kuahidi wananchi wa kaunti hiyo angeuleta hapo mbeleni lakini ameutimiza mradi huo.

Kwa upande mwingine wakaazi wa Nyamaiya warifurahia mradi huo huku wakimwomba seneta huyo kuanzisha mradi mwingine ijapo wa mikopo ambayo itawasaidia pakubwa.

“Tunampongeza Seneta Okong’o kwa yale anayafanya lakini tunahitaji kujiendeleza kimaisha na kumwomba seneta aanzishe mradi wa mikopo ambayo itatuwezesha kufanya biashara ili tujiimarishe kimaendeleo,”aliomba Jackline Kemunto Nyakundi.