Mkuu wa Idara ya Ardhi Kaunti ya Mombasa Antony Njaramba amesema kuwa serikali ya kaunti iko tayari kushirikiana na serikali ya kitaifa katika kumaliza mizozo ya ardhi inayowakumba wakaazi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Njaramba amesema kuwa idara yake inajitahidi katika kumaliza mizozo ya ardhi ili wakaazi waweze kumiliki ardhi zao kisheria.

“Tuko tayari kufanya kazi na serikali ya kitaifa katika kuangamiza mizozo ya ardhi eneo la Mombasa,” alisema Njaramba.

Akizungumza siku ya Jumatatu kwenye kikao na Waziri wa Ardhi Jacob Kaimenyi, Njaramba alisema kuwa watakabiliana na mabwanyenye wanaonyakuwa ardhi za wananchi wasiojiweza pamoja na kuhakikisha kuwa wanachukuliwa hatua za kisheria.

“Tuko imara kuwakabili hawa mabwanyenye wanaowaangaisha wananchi kwa kunyakua ardhi zao,” alisema Njaramba.

Aidha, amesema kuwa Kaunti ya Mombasa iko na takriban maskwota kati ya laki moja hadi laki moja unusu.