Wakazi wa kaunti ya Nyamira wamepata sababu ya kutabasamu baada ya serikali ya kaunti hiyo kuajiri wahudumu 155 wa afya kwa ushirikiano na shirika la Aphia Plus.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubu kwenye hafla ya kuwapokeza wahudumu hao barua za uajiri kwenye shule ya upili ya Kebirigo siku ya Jumanne, gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama aliwaonya vikali wahudumu hao dhidi ya kuzembea kazini. 

"Wajibu ambao mmetuikwa hii leo ni wakuhakikisha kwamba mnawapokeza wakazi wa kaunti hii huduma bora za afya na sharti muwajibike kazini," alisema Nyagarama. 

Nyagarama aidha aliwaonya wahudumu hao dhidi ya kujihuzisha na visa vya ufisadi huku akiwarahi kujua hali zao za afya.

"Huenda wengine wenu mkajaribu kujihusisha na visa vya ufisadi, ila yeyote atakayepatikana atachukuliwa hatua kali za kisheria, kwa minajili ya kupambana na maradhi hasa saratani na ukimwi, ni himizo langu kwenu kujua hali zenu za kiafya," aliongezea Nyagarama.