Serikali ya kaunti ya Kisii imehimizwa kufanya miradi ya maendeleo sawia kila sehemu ya kaunti hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wito huo umetolewa baada ya kudaiwa kuwa serikali hiyo haifanyi miradi ya maendeleo sawia kwa kila sehemu ya kaunti, jambo ambalo sasa limelaumiwa na baadhi ya viongozi pamoja na wakazi.

Akizungumza na mwanahabari huyu, mbunge wa eneo bunge la Mugirango kusini kaunti ya kisii Manson Nyamweya aliomba serikali ya kaunti kujaribu kila iwezalo kuhakikisha kila eneo bunge la kaunti hiyo limefanyiwa maendeleo sawia na maeneo mengine ya kaunti .

“Naomba gavana wa Kisii James Ongwae wakati anafanya maendeleo awe anafanya kila sehemu ya kaunti ili kuonyesha uwazi kwa wakazi wote wa kaunti ya Kisii,” alisema Manson Nyamweya.

Aidha, Nyamweya aliomba kaunti hiyo kuinua mji wa Ogembo kimaendeleo huku akisema mji huo kungekuwa na kaunti nyingine lakini ikaunganishwa na kisii ikawa moja na kuomba maendeleo yanayofanywa kisii yafanywe mji wa Ogembo pamoja na sehemu zingine .

“Tunahitaji mji wa Ogembo kuinuka kimaendeleo jinsi mji wa Kisii nayo imeinuka ili wakazi kufurahia matunda ya serikali za ugatuzi,” aliongeza Nyamweya.