Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Serikali ya kaunti ya Nyamira imehimizwa kuharakisha ujenzi wa soko la Nyabite eneo bunge la Mugirango magharibi ili kuruhusu wafanyibiashara wa soko hilo kufanya biashara zao bila kukumbwa na changamoto mbalimbali katika biashara zao.

Wito huo umetolewa baada ya ujenzi huo kuanzishwa hapo awali na kuchukua muda mrefu bila kukamilika na kupelekea wafanyibiashara kutopata mahali pa kufanyia biashara zao kwani huuzia kandokando mwa barabara.

Wakizungumza siku ya Jumanne katika mji wa Nyabite, wafanyibiashara hao walisema wamesumbuka sana kwa kufanyia biashara zao kando kando mwa barabara huku wakihofia kugongwa na magari yanapopita.

“Serikali ya kaunti imechukua muda mrefu kukamilisha ujenzi huu wa soko kwani tumekuwa tukifanyia biashara kandokando mwa barabara kwa wakati mrefu,” alisema Jackline Bosibori, mwanabiashara

Pia wafanyibiashara hao waliomba serikali hiyo kupanua soko hilo kuwa kubwa huku wakisema jinsi soko hilo linajengwa inastahili kupanuliwa ili wafanyibiashara wengi kupata nafasi ya kutosha na kufanyia biashara zao.