Wafanyibiashara wa jua kali katika kaunti ya Nyamira wameomba serikali ya kaunti hiyo kuwasaidia kujiendeleza na kuimarisha sekta hiyo ambayo wanaitegemea.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na wafanyibiashara hao, sekta ambayo inamiliki idadi nyingi ya wakazi ni jua kali na haiwezi kusonga na kuinuka bila usaidizi wa serikali.

Wakizungumza siku ya Jumanne mjini Nyamira, wanajuakali hao waliomba usaidizi kutoka kwa serikali kwa kuwafadhili ili kujiendeleza.

“Sekta hii yetu ni miongoni mwa sekta za biashara ambazo humiliki idadi kubwa ya wakazi na tunaomba kaunti kutusaidia ili nasi kujinufaisha kutokana na biashara zetu na tunaomba tufadhiliwe,” alisema Patrick Bosire, mkazi.

"Ikiwa tutasaidiwa tunaomba gavana wa kaunti hii John Nyagarama akumbuke sekta hii ili tujiimarishe kimaisha na tuinue uchumi wa kaunti hii yetu,” aliongeza Bosire.

Wakati huo huo, waliomba serikali kuwaleta wawekezaji kuekeza katika kaunti hiyo ili kuwanufaisha zaidi kupitia ununuzi wa bidhaa zao.

Aidha, waliomba kaunti kununua fanicha na bidhaa zingine ambazo wanatengeneza ili kuwanufaisha huku wakisema mara nyingi serikali hugharamika kwa kununua bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi na kuwaacha.

“Tunahitaji kutosumbuliwa na askari wa kaunti ambao hutusumbua wakati wa ushuru ili kuinua sekta hii,” alisema Hesbon Nyagesiba, mwanajuakali mwingine.