Serikali ya kaunti ya Kisii imehimizwa kusaidia hospitali ya Kiogoro iliyoko eneo bunge la Nyaribari Chache kwa kuiunganishia nguvu za umeme ili kuimarisha huduma za matibabu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wito huo umetolewa baada ya nguvu za umeme kukatwa katika hospitali hiyo mwezi desemba mwaka jana, na kupelekea huduma za matibabu kutatizika kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza siku ya Jumatatu katika hospitali hiyo, mwenyekiti wa hospitali hiyo Meshack Anunda alisema tangu mwaka jana hakuna nguvu za umeme katika hospitali hiyo, na kupelekea shughuli nyingi za huduma kutofanyika kikamilifu.

Anunda alisema huwa wanalazimika kupeleka dawa katika hospitali zingine zilizoko karibu ambazo ziko na stima ili kuweka dawa kwa njia bora kutoharibika.

“Tunaomba serikali ya kaunti kutusaidia ili hospitali hii iboreshwe zaidi kimatibabu maana shughuli nyingi za matibabu zimetatizika pakubwa,” alisema Anunda.