Serikali ya kaunti ya Kisii imehimizwa kuwasomesha watu udaktari wa macho ili kuimarisha afya katika kaunti hiyo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa kuna upungufu wa madaktari wa macho katika kaunti ya Kisii ilihali wagonjwa wa macho wanaendelea kuongezeka kila uchao.

Akizungumza nasi daktari wa macho katika hospitali ya macho, Professa Dan Kiage alisema katika kaunti ya Kisii hakuna madaktari wa kutosha ili kushughulikia shida za macho na kuomba kaunti kuingilia kati na kuwapeleka baadhi ya watu kusomea taaluma hiyo ili kuwasaidia wakaazi ambao wana shida ya macho.

Kulingana na Kiage idadi kubwa ya watu ambao wana ugonjwa wa Kisukari, ugonjwa wa Ukimwi ndio huwa na shida ya macho na kusema idadi ya walio na shida hiyo imeongezeka na madaktari wa kuwashughulikia hawatoshi.

“Tunaomba serikali ya kaunti ikiwa inahitaji kusaidia watu walio na shida ya macho hapa Kisii iwapeleke shuleni baadhi ya watu ili kusomea matibabu ya macho," alisema Kiage.

Aidha, aliomba serikali ya kaunti ya Nyamira nayo kufanya hivyo hivyo huku akisema kuwa kati ya watu millioni mbili walioko eneo la Gusii watu 200,000 wako na shida ya macho na kusema mbinu sharti itafutwe ya kutoa matibabu kwao