Serikali ya kaunti ya Kisii imeombwa kujenga vituo vya kuweka mavuno kila eneo bunge la kaunti hiyo ili mavuno hayo kuwekwa mahala pazuri pa kutoaribika zaidi kama njia moja ya kupunguza janga la njaa.
Hii ni baada ya kusemekana kuwa hakuna vituo hivyo ambavyo vinaweza tumika kuwekeza mahindi, maharage na mavuno mengine mengi, jambo ambalo huchangia janga zaidi.
Chama cha kutetea haki za kibinadamu kwa jina ‘Kisii County Community Forum Kick off’ kiliomba jambo hilo liweze kuafikiwa ili kupunguza janga la njaa katika kaunti hiyo.
Victor Maina, mwanachama wa chama hicho alisema ikiwa serikali ya kaunti ya Kisii inahitaji kujali maslahi ya wakazi wa kaunti hiyo, sharti iweke mbele sekta ya kilimo ili kuimarika zaidi.
“Sisi kama chama cha kutetea haki za binadamu hapa Kisii tunaomba vituo vya kuweka mavuno kujengwa kila eneo bunge la kaunti hii ili njaa isiwe inashuhudiwa Kisii,” alisema Maina.
Ata hivyo, chama hicho kiliomba bunge la kaunti kutengeneza sheria za kuwazuia matapeli ambao wako katika masoko ya Kisii ambao hununua bidhaa kwa bei ya chini na kupeleka katika miji mikuu ili kujinufaisha