Serikali ya kaunti ya Kisii imehimizwa kutengea sekta ya kilimo pesa nyingi ili kuinua na kuimarisha zaidi sekta hiyo katika kaunti hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya kubainika kuwa idadi kubwa ya wakazi wa Kisii hutegemea kilimo, huku kaunti ya Kisii ikiombwa kujali maslahi ya wakazi hao na kutenga pesa nyingi kwa sekta hiyo.

Chama cha kutetea haki za kibinadamu kwa jina ‘Kisii County Community Forum Kick off’ kilisema kilimo ni sekta ambayo imeleta umaarufu kwa kaunti ya Kisii, na kuomba kutengewa asilimia 10 ya pesa katika bajeti ya mwaka unaofuata ili kuendeleza kilimo.

Akizungumza na huyu mwanahabari, mwanachama wa chama hicho Victor Maina alisema kaunti ya KLisii itaendelea kunoga zaidi kupitia kilimo ikiwa serikali hiyo itajitolea kuisaidia.

“Hapa kisii wengi wetu ni wa kutegemea kilimo na kuendelea kusonga mbele, sharti serikali itenge pesa nyingi kwa kilimo, na ninaomba hayo kuafikiwa,” alisema Maina.