Mwakilishi wa wadi ya Bokimonge kaunti ya Kisii George Bibao ameomba serikali ya kaunti ya Kisii kutengeneza daraja ambazo ziliharibiwa na mvua wakati w mvua kubwa mwaka jana. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulingana na Bibao, kuna daraja nyingi ambazo ziliharibiwa wakati huo wa mvua kubwa, na imekuwa kikwazo kwa wakazi ambao wameshindwa kutumia vivukio hivyo. 

Akizungumza siku ya Jumanne mjini Kisii, Bibao alisema serikali ya kaunti hiyo ilitenga millioni 50 ambazo zingegharamia mikasa ambayo ingesababishwa na mvua ya masika El Nino, huku akisema pesa hizo zitumike kutengeneza daraja hizo.

Bibao aliomba daraja la Tongeri katika wadi yake kutengenezwa baada ya kufagiliwa na mvua hiyo, jambo ambalo amesema limewaathiri wakazi wa eneo hilo ambao wameshindwa kutumia daraja hilo. 

“Sisi kama wawakilishi wa wadi tulitenga pesa shillingi millioni 50 ambazo zingeshughulikia mikasa yote ingesababishwa na mvua ya El Nino. Naomba serikali kutumia pesa hizo kutengeneza daraja zilizoaribiwa na mvua,” alisema Bibao.

Aidha, mwakilishi huyo alisema amepokea ripoti kuwa barabara zilizoaribiwa na mvua hiyo zitatengenezwa hivi karibuni kupitia serikali ya kaunti hiyo ya Kisii na kupongeza hatua hiyo.

Picha: Mwakilishi wa wadi ya Bokimonge George Bibao. Ameomba serikali ya kaunti ya Kisii kutengeneza daraja ambazo ziliharibiwa na mvua ya Eli Nino. Maktaba