Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kaunti ya Kisii imeanzisha mradi wa kupandisha hadhi zahanati zote katika kaunti hiyo hadi kiwango cha level 4 ili kuimarisha sekta ya afya.

Hii ni baada ya kubainika kuwa idadi kubwa ya zahanati katika kaunti hiyo hazina huduma zinazostahili huku zikianza kupandishwa hadhi ili sekta ya afya iimarike zaidi katika utoaji wa huduma bora kwa wakaazi.

Akizungumza katika zahanati ya Kenyerere iliyoko eneo la Nyamache eneo bunge la Bobasi kaunti ya Kisii waziri wa afya Sarah Omache alisema kuwa zahanati zote za kaunti hiyo zitapandishwa hadhi ili kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa.

“Huduma za matibabu si bora katika zahanati na serikali ya kaunti imeanza kuzipandisha hospitali hizo hadhi ili kuimarisha afya zaidi kwa kaunti yetu,” alisema Omache.

Wakati huo huo, zahanati ya Kenyerere ilipandishwa hadhi hiyo jana hadi kiwango cha level 4 huku ikitarajiwa sekta ya afya itaimarika zaidi.