Mkuu wa Idara ya Elimu katika Kaunti ya Mombasa Tendai Lewa amepinga pendekezo la kubadilishwa kwa mfumo wa masomo wa 8-4-4 hadi 2-6-6-3.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa siku ya Alhamis baada ya kuhudhuria kongamano la wadau wa sekta ya elimu mjini Mombasa, Tendai alisema kuwa wadau wa Sekta ya Elimu wanafaa kubuni vitengo vya kukuza talanta na kusisitizia wanafunzi kufanya bidii zaidi katika baadhi ya masomo.

Lewa alisema kuwa kubadilishwa kwa mfumo huo kutazidi kudidimiza viwango vya elimu nchini, kwani masomo ya darasa la nane yanaumuhimu mkubwa kwa mwanafunzi.

Mkuu huyo wa idara amewataka wadau wa sekta ya elimu, Waziri ya Elimu nchini Fred Matiangi na bodi inayoshughulikia maswala hayo kuwa waangalifu ili kuzuia kuharibika kwa mfumo wa elimu nchini.

"Sisi bado hatujaridhishwa na mipango inayoendelea kwa sasa ya kubadilisha mfumo wa elimu na kuleta mwengine mpya. Hatua hiyo ni kama inahujumu jukumu la mwanafunzi darasani kwa kuwa hata viongozi hao hawajajumuisha wananchi katika mchakato huo kufahamu maoni na mapendekezo yao,” alisema Tendai.