Serikali ya Kaunti ya Mombasa imehimizwa kutafuta njia mwafaka ya kukusanya ushuru wa wakaazi wa kaunti hiyo.
Haya ni kwa mujibu wa Job Sitima, ambaye ni msemaji wa Shirika la vijana katika Kaunti ya Mombasa la Youth Center.
Akizungumza siku ya Jumatano mjini Mombasa, msemaji huyo alisema kuwa kwa muda mrefu kitengo kinachohusika na sekta hiyo kimekuwa fisadi hali aliyoitaja kuhujumu bajeti ya serikali hiyo.
Sitima alisema kuwa hatua hiyo hufanya mugao wa fedha kuwa hafifu mno kwani sekta hiyo haitekelezi matwaka yake ipasavyo.
Haya yanajiri huku serikali ya Kaunti ya Mombasa ikiwa na pendekezo la bajeti ya shilingi bilioni tisa nukta tano.