Kufwatia tukio la moto lililotekea katika shule ya Nyasabakwa katika kaunti ya Nyamira siku ya Alahamisi asubuhi, kaunti ya Nyamira imetoa msaada wa dharura.
Akizungumza na waandishi wa habari, katibu wa kaunti Eric Onchana alisema kwamba iliwalazimu kununua baadhi ya vitu vya malazi ili kusaidia waadhiriwa.
"Sisi kama kaunti baada ya kuarifiwa kuhusu mkasa huu imetulazimu kuwanunuliwa waadhiriewa wote mito, blanketi, sanduku na ata vitambaa vya vitanda ili kusaidia hawa wanafunzi," alisema Onchana.
Kulingana na afisa huyo, kaunti ilitumia takilibani laki saba kununulia wanafunzi 120 bidhaa hivyo.
"Tumetumia elfu mia 700 kununa hivi vitu vyote vilivyochomeka ili kupunguza wazazi gharama ya kuvinunua," aliongeza.
Vile vile kaunti ilihahidi kuendelea kusaidia shule hiyo kujenga bweni jingine mpya na la kisasa.
Maafisa wengi wa kaunti walihudhuria akiwemo bibi ya gavana wa kaunti Naomi Nyagarama, waziri wa elimu na waziri wa fedha na wengine wengi.
Kiini cha tukio hilo la bado hakijatambulika huku uchunguzi ukiendelea.