Waziri wa kilimo wa kaunti ya Nakuru Stanley Chepkwony amesisitiza ya kwamba kaunti hiyo inauwezo wa kujitosheleza kwa chakula iwapo wakulima watazingatia kikamilifu ushauri wa wataalam wa kilimo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na waandishi wa habari alhamisi wakati wa kikao cha matayarisho ya maonyesho ya kilimo ambayo yatafanyika kati ya julai 5-9, Chepkwony amewataka wakulima kufanyiza kazi ushauri wa wataalam ili waweze kupata mazao bora.

"Ujumbe tunaotaka kufikisha kwa wakulima na hata pia wafanyibiashara na kwa wakaazi wa Nakuru ni kuwa wanafaa kutafuta nafasi kutembelea maonyesho ya kilimo kwasababu kwa kuwa watapata msunfo mengi," alisema wziri huyo.

Ameashiria kuwa ingawa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa hili, amewataka wakulima watumie maonyesho hayo ya kilimo kupata mafunzo ya kuboresha kilimo chao.

’Kuna kampuni zilizo na mbegu mpya huku zingine zikiwa na mashini zitakazotumika kwenye shamba. Wengine pia awanatengeza vifaa mbalimbali za kisasa. Ni lazima wakulima watafute sababu iliyopelekea vibanda hivyo kuwepo hapo na kwa kufanya hivyo, watafaidika kileimu," aliongeza waziri.

Ikiwa mauthui ya mwaka huu ni kutumia teknologia katika uzalishaji wa mazao ya kilimo, Chepkwony alisisitiza kwa kufanya hivyo mkulima ataweza kujitosheleza kwa chakula na kisha kuweza kuuza mazoa mengine.

Zaidi ya wafanyibiashara sabini wamedhibitisha kushiriki katika maonyesho hayo ya mwaka huu, hapa mjini Nakuru.