Afisa mmoja wa polisi alibubujikwa na machozi akihojiwa na tume ya kitaifa ya huduma za polisi inayo piga msasa maafisa wa polisi. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Afisa huyo,Joshua Aseto alianza kutiririkwa na machozi pale tume hiyo ilimtaka aelezee kuhusu mamilioni ya pesa iliyoko katika akaunti yake.

Kwa sasa tume hiyo imepiga kambi katika Kaskazini mwa Bonde la ufa, kaunti ya Uansin Gishu mjini Eldoret. 

Zoezi hilo linatarajiwa kukamilika siku ya Alhamisi linawashirikisha maafisa wote kutoka vitengo vyote vya polisi nchini.

Kulingana na mwenyekiti wa kitaifa katika tume hiyo Johnstone Kavuludi, shughuli hizo zinatarajiwa kuboresha utendaji kazi katika sekta ya polisi.

Kavuludi aliwataka maafisa ambao hawajahojiwa kuwa na subira wakati shughuli hizo zinaendelea. Kavuludi aliongeza kwamba wale watakao hitimu wataendeleza majukumu yao na wale ambao hawatapita basi wataachwa nje ya tume.

Miongoni mwa waliohojiwa ni Ahmed Idle ambaye alisema kwamba kwa eneo lake la kazi hajashuhudia ufisadi wowote na amepongeza maafisa wa polisi kutoka sehemu hiyo ya kaunti ndogo ya Kidisha katika kaunti ya Turkana.

Vile vile alitaka bodi hiyo kuzingatia ombi lake la maafisa wanaohudumu kwa sehemu kame kuongezewa fedha za kujikimu na afisa yeyote akipatikana na kosa sheria ichukue mkondo wake.

Aidha,Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu amepongeza tume hiyo kwa shughuli hizo kwa sababu ni mwelekeo wa kiteknolojia. Mandago aliongezea kuwa hatua hiyo itasaidia wananchi kuwa na imani na maafisa wa polisi.