Mkurugenzi mtendaji wa shirika la kukadiria ubora wa bidhaa nchini KEBS Charles Ongwae anasema shirika hilo limefunga zaidi ya kampuni themanini za kutengeza maji ya kunywa nchini.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza wakati wa warsha na wanahabari mjini Naivasha Jumamosi, Ongwae alisema kwamba wanawajibu wa kuhakikisha wakenya wanatumia bidhaa salama ikizingatiwa kuwa uwepo wa maji safi na salama ya kutumia ni mojawapo ya mahitaji muhimu kikatiba.

Kadhalika, aliongeza kwamba kufikia sasa, ni kampuni mia sita pekee ambazo zimesajiliwa na kuidhinishwa na shirika hilo.

Kulingana na afisa huyo wa KEBS, kuna kampuni nyingi zinazoendesha shughuli zao za kutengeza bidhaa kinyume cha sheria akidhibitisha kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu, watakuwa wamezifunga na wahusika kufikishwa mahakamani.