Shirika la kukadiria ubora wa bidhaa nchini Kebs limefunga zaidi ya kampuni 80 za kutengeneza maji ya kunywa. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na ripoti kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa Kebs, Charles Ongwae amesema maji ni mojawapo ya bidhaa muhimu na hivyo basi wana wajibu wa kuhakikisha wakenya wanatumia bidhaa zilizo salama. 

Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa kufikia sasa  kampuni 600 ambazo zimesajiliwa na kuidhinishwa na shirika hilo,ingawa kuna kampuni nyingi zinazoendesha shuguli zao za kutengeneza bidhaa kinyume cha sheria,na kuwa kufikia mwisho wa mwezi Disemba kampuni hizo zitakua zimefungwa zote.

Hii inafuatia baada ya kampuni nyingi nchini kubainika kuwa zinafanya biashara bila kutimiza masharti ya Kebs na miongoni mwa kampuni hizo zinauza bidhaa bandia ambazo husababisha magonjwa kwa wakenya. 

Hii inanuia kupunguza magonjwa kutokea haswa ikizingatiwa kuwa afya ya watu kote nchini itaimarika iwapo bidhaa zilizoidhinishwa na Kebs kama vile maji yametibiwa kabla ya kuuziwa wateja.