Mbunge wa Kieni Kanini Kega aliwaongoza wabunge kwenye maazishi ya mwanamziki Salim Junior kuahidi kuwa watahakikisha wasanii pamoja na kazi yao wanalindwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubia umati uliokuwa umehudhuria mazishi hayo siku ya Jumanne huko Subukia Nakuru, Kega alisema wanamziki pamoja na familia zao wamekuwa wakiteseka licha ya kufanya kazi nzuri.

“Nitawaongoza wabunge kubuni sharia itakayowalinda wanamziki pamoja na kazi zao. Mbunge yeyote atakayekosa kuunga mkono mswada wangu mhakikishe hamjampigia kura,” Kega alisema.

Mwanamziki mashuhuri Njoroge Muigai alisema kuwa wanasiasa wamekosa kuangazia shida za wanamziki licha ya kuwatumia wakati wa kampeni zao.

“Sisi pia tumechoka kutumiwa na watu ambao wakichaguliwa hawatujali. Wakifika bunge wanatusahau … sasa tumeelevuka,” Muigai alisema.

Aidha shirika la kushughulikia haki za wanamziki la Music Copyright Society (MCS) lilishtumiwa kwa kuwanyanyasa wanamziki. Mwanamziki Salim Junior alisifiwa kwa weledi wake kwenye miziki aina ya Kikuyu ambayo amekuwa akiimba kwa mtindo wa kipekee.