Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baraza kuu la waislamu humu nchini Kemnac limepinga kauli ya mbunge wa Rarieda Nicholas Gumbo, ya kutaka mkuu wa majeshi nchini Samson Mwathethe kujiuzulu.

Akiwahutubia wanahabari siku ya Jumatatu katika hoteli moja mjini Mombasa, mwenyekiti wa baraza hilo Sheikh Juma Ngao, aliyataja madai hayo kuwa ya chuki na uchochezi.

Sheikh Ngao alidai matamshi ya kiongozi huyo ni ya kutaka kumdhalilisha mkuu huyo wa jeshi.

Aidha, mshauri mkuu wa baraza la Kemnac Juma Abdulrazak alimtaka Gumbo kuomba msamaha dhidi ya matamshi yake.

Kauli hii inajiri baada ya Gumbo kumtaka mkuu wa majeshi nchini kujiuzulu baada ya kambi ya jeshi ya El Adde nchini Somalia kushambuliwa, huku wanajeshi wa KDF wakiuwawa.