Wanasiasa wengi wamekuwa wakiunga msimamo wa rais Uhuru Kenyatta kutaka Kenya ijiondoe katika mkataba was Roma ulioibuni mahakama ya ICC.

Share news tips with us here at Hivisasa

Jambo hili halifai na lahitaji kufanyiwa udadisi kwa kina. 

Chini ya mkataba huu, mtu, hasua kiongozi yeyote anayekosa na kushinda mamlaka ya nchi yake anaweza kufikishwa mbele ya mahakama hii na kuhukumiwa kama alivyofanyiwa aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor.

 Mkataba huu unahakikisha kuwa, mbali na kuwa na mamlaka, binadamu wote in sawa na haki za binadamu zinafaa kuheshimiwa. 

Mbali na kutupilia mbali kesi za Wakenya sita waliokuwa wameshitakiwa katika mahakam hiyo, haimaanishi ICC inawadhulumu waafrika kwa kuwahusisha na makosa bandia bali inamaanisha upande wa mashtaka hauku wajibiki vilivyo.

Hii inaleta haja ya kutilia mkazo kuwa mahakama hiyo ina vipengee tofauti ambavyo ni huru.

Kenya inafaa kushurutisha upande wa mashtaka ufanyiwe marekebisho kuliko kujiondoa kama mwanachama.

Ikiwa Kenya itajiondoa, kuna hatari ya uongozi wa kiimla kutokea maana rais yeyote atakayekuwa mamlakani ndiye kamanda was vikosi vyote vya usalama nchini. 

Rais yeyote anaweza kuamuru vikosi hivyo kumlinda kutokana na kukosolewa ikizingatiwa kuwa umoja was kimataifa utaingilia kati kuleta tu amani wala sio kukosoa sehemu yoyote ya mzozo.

Kabla ya wabunge kutaka Kenya ijiondoe kwa mkataba wa  Roma, wanafaa wapige darubini kwa siku zijazo na watakaokuwa. 

Wanafaa wajue kwamba ingawa kujiondoa kuna manufaa, kubaki kuna manufaa zaidi.