Kenya imekubaliana na Uingereza kushirikiana kikamilifu katika juhudi za kukabiliana na magaidi ili kuhakikisha kuwa wananchi wanalindwa na usalama uimairishwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kwenye taarifa ilitumwa kwa vyombo vya habari kutoka Ikulu ya Rais jijini Nairobi siku ya Ijumaa, baada ya mazungumzo baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Waziri wa maswala ya kigeni wa Uingereza Philip Hammond, viongozi hao wawili wamekubaliana kushirikiana kuimarisha usalama.

Rais Kenyatta amesema kuwa maswala muhimu yanahitaji kuangaziwa zaidi sambamba na kuwapa vifaa vya kisasa maafisa wa jeshi la AMISON nchini Somalia ili kukabiliana kikamilifu ya Kundi la Kigaidi la Al-shabab.

“Ni lazima tujitolee kikamilifu katika kukabiliana na magaidi hasa Alshabab na kuwapa wanajeshi wa AMISON motisha na ushirikiano wetu utaimarisha usalama wa Kenya na amani nchini Somalia”,alisema Rais Kenyatta.

Kwa upande wake Waziri Hammond amesema kuwa serikali ya Uingereza itajitolea kikamilifu katika kuisaidia Kenya kudhibiti ugaidi, huku akiahidi kuhakikisha kuwa taifa la Somalia linakuwa na amani.

Waziri Hammond ameonekana kukosoa hatua ya Mrengo wa Cord kuhusu Maandamano, akisema kuwa kuna umuhimu wa kufuata sheria katika kusuluhisha maswala yanaoangaziwa wananchi.

Mazungumzo hayo yaliwajumuisha mawaziri na viongozi wengine serikalini ikiwemo Waziri wa Maswala ya kigeni nchini Bi Amina Mohammed na Waziri wa maswala ya ndani Joseph Nkaissery.