Hisia mseto zinazidi kuibuka mjini Mombasa kutokana na idadi ya watu ambao walifariki kwenye mkasa katika jumba la mkasa wa huruma jijini Nairobi siku nane zilizopita.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi wanazidi kujiuliza maswali ni vipi watu waneza achwa kufariki kiholela kwa kutokana uzembeaji wa watu kwenye kazi zao.

Watu wanapaswa kupata mafunzo kutokana na mikasa kama hii, kwani visa kama hivi sio mara ya kwanza kushudiwa hapa nchini.

Hapo miaka ya nyuma huko jijini Nairobi hali kama hiyo iliweza kushuhudiwa na kilichotokea ni vurugu la nyumba kuvujwa na hatimaye mambo hayo kuisha hivyo.

Pindi tu wanahabari wanapoacha kuangazia swala hilo basi huzikwa kwenye kaburi la sahau na hatimaye jambo kama hilo linapoibuka tena ndio watu hukumbuka kuwa unjenzi wa nyumba lazima ufuate vigezo vyake.

Idadi ya watu waliofariki katika mkasa wa Huruma imefika 44.

Ni baada ya watu wengine wanne kuondolewa mapema leo kutoka jengo hilo lililopormoka siku 8 zilizopita.

Mkuu wa polisi hapa Nairobi Japheth Koome, amesema watu 140 wameokolewa kufikia sasa na kwamba bado waokoaji wanamatumani ya kupata waathiriwa zaidi wakiwa hai.

Kufikia sasa watu 70 bado hawajulikani waliko juma moja baada ya jumba kuporomoka.