Juhudi za kusambaza maji katika Kaskazini mwa Kenya imepata msaada zaidi baada ya serikali ya Saudi Arabia kutoa msaada ya sh500 milioni.
Kulingana na waziri wa maji na unyunyizaji, Eugene Wamalwa, msaada huo utatumika katika mashule ya msingi nchini ambayo itaanzia shule za kaunti kaskazini mwa Kenya ambayo ni pamoja na kaunti za Garissa, Wajir na Mandera.
Akipongeza juhudi za serikali ya Saudi, mwalikilishi bunge wa Garissa, Aden Duale alikutana na washauri wa msaada wa Saudi ya maendeleo (Saudi Fund for Development), wakiongozwa na Ibrahim Alturki.
Duale alizungumza na wadhamini hao kutoka mashariki ya kati ambao pia walichangia katika uundaji wa barabara ya Thika hadi Garissa na Nuno Modogashe wakisaidiana na serikali ya Kenya na kuwashukuru kwa ushirika wa nchi ya Saudi na Kenya katika maendeleo.