Maafisa wapya waliochaguliwa katika Huduma ya Kazi kwa Vijana (NYS) wameombwa kushirikiana na serikali ya kitaifa kufanikisha na kusongesha mbele huduma hiyo ili kuwafaidi vijana.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika eneo la Nyagesenda eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazi, Rais Uhuru Kenyatta alisema ushirikiano ndio utafanikisha huduma hiyo.
Ata hivyo Kenyatta aliwatahadharisha maafisa hao dhidi ya kuhusika na visa vya ufisadi baada ya kubainika kuwa maafisa waliokuwa katika huduma hiyo walidaiwa kuhusika kwa ufisadi jambo ambalo lilipelekea huduma hiyo kutoendelea.
“Naomba tushirikiane tusaidie vijana wetu nao waweze kujiendeleza kupitia kazi ile watafanya ya NYS na kusonga mbele katika maisha yao,” alisema Kenyatta.
“Lakini ikiwa ufisadi utaingizwa tena hatua za kisheria zitachukuliwa maana huduma hii ya NYS ilikosa kuendela mbele baada ya ufisadi kuiangusha,” aliongeza Kentyatta.
Wakati huo huo, Kenyatta aliomba wakaazi wa Kisii kushirikiana na serikali ya Jubilee kuhakikisha maendeleo mengi huku akiahidi kufanya maendeleo mengi katika jamii ya Kisii.