Rais Uhuru Kenyatta amepongezwa kwa usemi wake kuwa serikali yake itajenga hospitali za Level 4 na 5 katika kila kaunti ili kuimarisha sekta ya afya.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakizungumza nasi mjini Kisii wakaazi wa kaunti hiyo wakiongozwa na Titus Mose na Daniel Maobe walimpongeza Kenyatta kwa kusema kuwa serikali itahakikisha huduma bora za matibabu zinatolewa kote nchini kupitia ujenzi wa hospitali za Level 4 na 5.

“Sekta ya afya ni ya muhimu sana lakini kile Rais kenyataa alisema ni cha muhimu maana aliahidi kuwa kila kaunti itajengewa hospitali na kuweka vivaa vya matibabu na tunashukuru kwa hilo na tunaomba Rais aendelee kutoa usaidizi wa aina hiyo,” alisema Mose.

Kenyatta aliyasema hayo alipokuwa anasoma hotuba yake bungeni huku akisema kabla ya mwaka huu kukamilika hospitali nyingi nchini zitakuwa na mashine za kuosha damu ili watu kupata matibabu .

Wakati huo huo, wakaazi hao walifurahishwa kwa kuondolewa kwa ushuru kwa wakulima wa kahawa ili kilimo hicho kipate kuinika.