Richardson Clyde Roller akiwa kizimbani hapo awali. [Picha/ standardmedia.co.ke]
Mahakama ya Mombasa imemuachilia huru afisa wa zamani wa kitengo cha FBI huko Marekani, anayekabiliwa na madai ya kupatikana na silaha kinyume cha sheria.Richardson Clyde Roller anadaiwa kupatikana na bunduki katika nyumba yake eneo la Nyali mnamo Machi 19, mwaka huu.Roller aliondolewa mashtaka hayo yaliyokua yakimkabili baada ya afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kuwasilisha barua mahakamani ya kutaka kesi hiyo kufutiliwa mbali.Hakimu mkuu katika Mahakama ya Mombasa Evans Makori alitupilia mbali kesi hiyo baada ya kukabidhiwa barua hiyo.Barua hiyo ilisema kuwa kulingana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani ni wazi kuwa silaha hizo hazikupatikana katika nyumba ya Roller.