Kesi ya mfanyabiashara mmoja mjini Mombasa imeahirishwa baada ya Jaji Patrick Otieno kusema kuwa hayuko tayari kusikiza kesi hiyo.
Mfanyabiashara huyo, Ashok Dosh, aliishtaki benki kuu ya CBK pamoja na benki ya Imperial kwa kutomlipa pesa zake shilingi bilioni moja kabla ya benki hiyo kuwekwa chini ya urasimu.
Wakili wa Dosh, Francis Kadima, alikashifu hatua ya benki kuu kuagizia mteja wake kulipwa shilingi milioni moja kwa kila mwezi.
Hata hivyo, mahakama ilisamamisha mfumo wa benki hiyo kutaka kulipa wateja wake pesa pole pole hadi kesi ya Dosh itakaposikizwa na kuamuliwa.
Wakili wa benki za Imperial na CBK kutoka jijini Nairobi walifika katika Mahakama ya Mombasa siku ya Ijumaa kusikiza kesi hiyo.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi tarehe 25 mwezi Mei.