Kesi ya wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Nyamagwa walioshtakiwa katika mahakama ya Ogembo ilikosa kuendelea siku ya Jumatatu baada ya upande wa mashtaka kukosa kuwasilisha ripoti za ushahidi kwa wakili wa wanafunzi hao na kusababisha kesi hiyo kuhairishwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wanafunzi hao wanane walishtakiwa kwa madai ya kuchoma bweni la shule jambo ambalo liliwapelekea kushtakiwa katika mahakama ya Ogembo

Wakati huo huo, wakili wa wanafunzi hao Ombui Mogire aliomba mahakama hiyo kuagiza wasimamizi wa shule kuwaruhusu wanafunzi hao kuchukuwa bidhaa zao kutoka shule hiyo huku akiomba mwalimu mkuu wa shule hiyo Florence Osoro kuwapa wanafunzi hao barua ya kujua hatima yao iwapo watarudi shule hiyo au la.

“Tungependa kujua ikiwa wanafunzi hawa wataruhusiwa kurudi shule au la,” alisema Mogire.

Jaji wa mahakama hiyo Caroline Ateya aliagiza mwalimu mkuu wa shule hiyo kufikishwa katika mahakama hiyo ya Ogembo Aprili 20.

Kesi ya wanafunzi hao itasikizwa tena mnamo agosti 9, 2016.