Kesi mbayo Mbunge wa Kitutu Masaba Timothy Bosire, ana ishtaki serikali kwa kupunguza walinzi wake itasikizwa hivi leo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge Bosire alienda mahakamani baada ya Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaisery kupunguza idadi ya walinzi wake.

Katika hukumu yake, Jaji Isaac Lenaola alisema kuwa kumpokonya Bosire afisa wa usalama ni kinyume na sheria, na akaamuru walinzi wake kurudishwa.

Kwa upande wake Bosire alidai kuwa uamuzi wa kumpokonya walinzi uliafikiwa pale alipokataa kutii agizo la Rais Kenyatta alipoamuru wasimame kwa ishara ya heshima kwa majeshi waliouawa eneo la El Ade, Somalia. 

Alielezea kuwa alikataa kusimama kwa sababu serikali ilikataa kutoa habari za kweli kuhusiana na mauaji hayo.