Kesi ya familia mbili zinazo zozania kuzika mwili wa msichana wa miaka 22 aliyefariki katika eneo la Mtwapa itasikizwa na Hakimu Henry Nyakweba.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Haya yanajiri baada ya mahakimu watatu kudinda kusikiza kesi hiyo.

Mahakimu Simon Rotich, Julius Nang’ea na Douglas Ogoti walijitoa kwenye kesi hiyo kwa sababu za kibinafsi.

Familia ya Isaac Njoroge na Zainabu Isaac zimekuwa zikizozania kuzika mwili wa Yasmini Njoroge, mwenye umri wa miaka 22, aliyefariki tarehe 11 mwezi Machi mwaka huu.

Akitoa uamuzi wake siku ya Jumatano, Hakimu Nyakweba alisema kuwa kesi hiyo ni ya dharura na itaendelea kusikizwa tarehe 26 mwezi huu.

Wakili wa mshtakiwa katika kesi hii Isaac Njoroge, ameiambia mahakama kuwa atawasilisha mashahidi wake wawili siku ya Alhamisi.

Familia hizo zinataka kuuzika mwili wa binti huyo kulingana na dini zao tofauti.

Mwili wa marehemu unahifadhiwa katika Hospitali kuu ya ukanda wa Pwani.