Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo. Kesi ya kupinga ushindi wake yasikilizwa leo. [Picha: sde.co.ke]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kesi ya kupinga ushindi wa mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi itasikilizwa siku ya Jumatatu wiki ijayo.

​Hii itafuatia ile ya mbunge wa Kisauni Ali Mbogo ambayo imeanza kusikilizwa leo katika mahakama kuu ya Mombasa.

Kesi hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa Agosti nane.

Bedzimba anadai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu mwingi na anaitaka Mahakama kubatilisha ushindi wa Mbogo.

Bedzimba alipata kura 29,752, huku Mbogo akiibuka mshindi kwa kupata kura 34,898.