Mbunge wa Jomvu Badi Twalib katika hafla ya awali. [Picha/ the-star.co.ke]
Mahakama kuu ya Mombasa imetupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Jomvu Badi Twalib.Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mkaazi mmoja wa Jomvu, Jimmy Mkala Kazungu.Mahakama imesema kuwa kesi hiyo imekosa kutimiza vigezo muhimu vinavyohitajika kwenye kesi za uchaguzi, kwa mujibu wa katiba.Akitoa uamuzi huo, Jaji Mugure Thande alisema kuwa kesi hiyo haiwezi kusikizwa kwa kutotimiza kanuni hizo.Kulingana na sheria, kesi za uchaguzi zinapaswa kuweka wazi tarahe ya uchaguzi, matokeo rasmi ya uchaguzi, pamoja na tarehe ambayo mshindi wa uchaguzi alitangazwa.Jaji Thande alisema kesi hiyo itatupiliwa mbali kwa vile ilikosa kutimiza vigezo hivyo vyote.