Mahakama ya Mombasa imesimamisha kwa muda usiojulikana kesi ya mshukiwa mkuu wa ugaidi Samantha Lewthwaite baada ya idara ya usalama kushindwa kumtia mbaroni.
Siku ya Jumatano, hakimu katika mahakama ya Mombasa, Julius Nang’ea, alisema kuwa mahakama haitaitaja ama kusikiliza kesi hiyo hadi pale mshukiwa huyo atakapotiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani.
Aidha, aliongeza kuwa agizo la kukamatwa kwake bado lipo licha ya kusimamishwa kusikilizwa na kutajwa kwa kesi hiyo.
Mshukiwa Samantha Lewthwaite na Mkenya Habib Saleh wanakabiliwa na madai ya kumiliki vilipuzi jijini Mombasa mnamo mwaka 2011.
Aidha, wanahusishwa na uvanizi wa jumba la Westgate ulisababisha mauwaji ya watu 67.