Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama ya mjini Kwale imetangaza kujiondoa kweye kesi ya uhalifu dhidi ya mwanawe mbunge wa Matuga Hassan Mwanyoha.

Hussein Mwanyoha, mwanawe mbunge huyo, pamoja na mwenzake walishtakiwa kwa kosa la wizi wa mabavu mapema mwaka jana.

Inadaiwa kuwa Mwanyoha alimtishia maisha na kumuibia simu na pesa mwanamume mmoja katika eneo la Diani huko Ukunda, mnamo Mwezi Machi mwaka jana.

Wawili hao walikana mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkaazi Cosmas Maundu.

Hakimu Maundu alisema kuwa kesi hiyo imehamishwa hadi katika mahakama ya Mombasa na inatarajiwa kuskizwa tena tarehe Februari, 16 katika mahakama hiyo.