Kesi ya ubakaji inayomkabili mganga anayedaiwa kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu imekosa kuendelea katika mahakama kuu ya Mombasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kesi hiyo imeahirishwa baada ya afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kusema kuwa haijajitayarisha kusikiliza rufaa hiyo.

Siku ya Jumatatu, Mwendesha Mashtaka Erick Masila kutoka afisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma aliiomba mahakama kumpa muda zaidi kupitia nakala za kesi hiyo.

Hatua hii inajiri baada ya mshukiwa huyo kupitia wakili wake Abdul Rahman Aminga kukata rufaa ya kuomba kuachiliwa kwa dhamana mbele ya Jaji Patrick Otieno.

Kati ya mwaka 2013 na Julai mwaka 2015 , Muhammed Ahmed anadaiwa kufanya mapenzi na mtoto huyo mdogo katika eneo la Bullo, Gatuzi dogo la Kisauni.

Kesi hiyo itasikilizwa Julai 15 mwaka huu.