Kesi inayowakabili vijana 22 waliokamatwa na maafisa wa usalama mnamo Februari 2, 2014 katika msikiti wa Masjid Musa jijini Mombasa iliendelea siku ya Jumatatu mbele ya Hakimu mkuu Douglas Ogoti.

Share news tips with us here at Hivisasa

Vijana hao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo kushukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la al-Shabaab, kumpokonya afisa wa usalama bunduki, kujitarisha kufanya uhalifu na kumiliki bunduki aina ya AK47 kinyume na sheria.

Aliyekuwa OCPD wa kituo cha polisi cha Makupa wakati wa oparesheni hiyo Bw Peter Mbua ambaye kwa sasa anahudumu kama komanda katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet, alitoa ushahidi wake dhidi ya washukiwa hao.

Wakili wa washtakiwa hao alishutumu upande wa mashtaka kwa kutoa ushahidi ambao haukuthibitishwa kurekodiwa katika kituo cha polisi na kuutaja kama ushahidi wa kubuniwa.

Miongoni mwa ushadi uliowasilishwa kotini ni silaha kama vile visu, panga na bunduki, paratakilishi, bendera zinazofananishwa na zile za al-Shabab pamoja na simu kadhaa za mkononi.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea leo (Jumannne) katika Mahakama ya Mombasa.