Kesi ya ugaidi dhidi ya wasichana watatu wakaazi wa Majengo, Kaunti ya Mombasa, ilikosa kusikizwa siku ya Jumatatu na kuhairishwa hadi Jumanne kwa madai ya upande wa mashtaka kukosa kuwasilisha shahidi katika kesi hiyo.
Wasichana hao waliokamatwa tarehe Juni 16, 2015 katika eneo la Mtwapa wakiabiri basi kuelekea Garissa walitambuliwa kama Nargis Arafat, Mwanajuma Tayari na Saumu Ali.
Watatu hao wanakabaliwa la shtaka la kupatikana na vifaa vinavyoweza kutumika katika shambulizi la kigaidi, walivyopokezwa na mwanaume mmoja aliyetorokea Uingereza, pamoja na kusudia kuvuka mpaka kwenda Somalia kujiunga na kundi la kigaidi la al-Shabaab.
Hakimu Diana Mochache aliamuru kesi hiyo kusikizwa siku ya Jumanne.