Shirika la Huduma za Feri nchini KFS limesema limeweka mikakati mipya ambayo itaboresha huduma katika kivuko cha Likoni.
Akizungumza afisini mwake siku ya Jumatano, afisa mkuu wa huduma katika shirika la KFS Elizabeth Wachira alisema kuwa feri zilikozoko kwa sasa huanza kuhudumu alfajiri ikilinganisha na hapo awali.
Aidha, alisema kuwa shirika hilo limeweka feri nne kuhudumu masaa ya asubuhi na jioni ili kusaidi katika kupunguza msongamano wa watu na kuwaimarishia wakaazi wa eneo hilo huduma za usafiri.
Bi Wachira pia alisema kuwa magari yanayowabeba watalii huvukishwa punde yanapofika kama njia moja wapo ya kuboresha sekta ya utalii.
Aliongeza kwa kusema kuwa kwa vile zaidi ya abiria laki tatu na magari zaidi ya elfu sita hutumia kivuko hicho cha feri, wataongeza idadi ya feri hadi saba kufikia mwisho mwa mwaka, ili kuboresha huduma za shirika hilo kwa wakaazi.