Wakaazi wa Kijiji cha Bosongo viungani mwa mji wa kisii wameelezea hofu yao juu ya kiangazi ambacho kimekumba eneo hilo tangia januari mwaka huu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hali hii imeathiri shughuli za kilimo, na hivyo kufanya maisha ya wakaazi kuwa magumu, huku wengi wao wakiwa wakulima ambao hujishughulisha na ukulima na ufugaji wa mifugo ili kukidhi mahitaji yao.

Moja ya shida zinazowakabili kwa sasa ni ukosefu wa maji, kwenye tukio ambalo lisilo la kawaida kwa wakaazi, kwani eneo hili linasifika kwa kupokea viwango vikubwa vya mvua kuliko maeneo mengine ya nchi.

Ukosefu wa maji umesababisha bei ya vyakula kupanda, kwani mboga hazipatikani kwa urahisi kama hapo awali.

Kulingana na mkaazi mmoja, Bw Omari, anaeleza jinsi ameathirika kwani hutegemea ng’ombe wa maziwa.

“Mapato yamepungua kwa kiwango kikubwa kwa sababu hakuna nyasi ya kumlisha ng’ombe wangu na hivyo kiwango cha maziwa kimepungua,” aeleza Bw. Omari.

Vilevile, upanzi wa mimea mbalimbali umeathiriwa pakubwa, kwani mpaka sasa wakulima bado hawajapanda na wale waliokuwa wameshapanda wanahesabu hasara kubwa.

Wafanyi biashara vilevile wameathirika, kwani imekuwa vigumu kupata bidhaa za kilimo kama kumkamua nyati.

Mmoja wa wafanyi bishara hao Bi Nyabuto anaeleza jinsi hali ya biashara inazidi kuwa ngumu kila uchao.

“Mimi nauza mboga na matunda, ni bayana kupata hizii bidhaa ni kizungumuti na huwa tunalipishwa bei ghali mno,” alieleza Bi Nyabuto.

Kubadilika kwa hali ya anga katika eneo hili huenda kukahatarisha uchumi wa kaunti ya Kisii katika siku za usoni.

Wakaazi wameumba uongozi wa Gavana Ongwae na Seneta Chris Obure, utoe suluhu la haraka ili kunusuru uchumi wa kaunti ya Kisii.