Mwenyekiti wa shirika lijulikanalo Grassroot women empowerment Grace Kibuku amewashtumu vikali baadhi ya wanasiasa wanaodaiwa kuwasafirisha wapiga kura kutoka sehemu moja hadi nyingine Kwa manufaa yao.
Kibuku anasema kuwa swala hilo ni la kusikitisha kwani wananchi hawafai kulazimishwa kujisajili popote bali ni shughuli inayofaa kuendeshwa Kwa uwazi.
"Ningependa kushtumu Kwa hali ya juu baadhi ya wanasiasa ambao baada ya kuona watashindwa wameanza kununua kura kwamba wakome kwani vyuma vyao vi Motoni," Kibuku alisema.
Wakati huo huo, aliitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kufanya uchunguzi wao kuhusiana na swala hili.
Kwa mujibu wa Kibuku ambaye ametangaza azma ya kuwania kiti cha mwakilishi wanawake Nakuru 2017, kiongozi yeyote anafaa kutii sheria ya uchaguzi na yeyote anayekiuka anafaa kuchukuliwa hatua Kali za kisheria.