Picha za nyama ya mbuzi. [okeymart.co.ke]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Idara ya afya kaunti ya Lamu imekifunga kichinjio cha nyama kaunti hiyo baada ya kukiuka kanuni za kiafya.

Maafisa kutoka idara ya afya na madaktari wa wanyama,wameshirikiana katika kikifunga kichinjio hicho cha nyama.

Akithibitisha kufungwa kwa kichinjio hicho afisa kutoka idara ya afya Athman Dumila, alisema siku ya Jumanne kuwa wamechukua hatua hiyo baada ya mazingara ya kichinjio kuwa machafu mno.

Aliongeza kuwa kichinjio hicho hakijaatimiza vigezo muhimu vya kanuni za afya,hatua aliyoitaja kuhatharisha afya ya wakazi wa Lamu.

Dumila amewataka wasimamizi wa kichinjio hicho kutimiza vigezo muhimu hitajika kama vile kuimarisha usafi, ili kuepeka maradhi ya kuambukiza kama vile kipindupindu.

Aidha, alitaja ukosefu wa maji na kuzagaa kwa taka taka katika maeneo ya kichinjio hicho ndio sababu kuu ya kukifunga.

Kwa upande wake Mahmoud Famau mwenyekiti wa Lamu meat market, amenyooshea kidole cha lawama kwa serikali ya kaunti ya Lamu kwa kushindwa kuondoa taka taka zinazopatikana karibu na kichinjio hicho.

Aidha, ameeleza kwamba kituo kinakumbwa na ukosefu wa maji, mazingira mabaya ya kuchinjia.

Famau amesema ni haki serikali ya kaunti kurekebisha hali katika kichinjio na kuhakikisha maji yanapatikana kwani wanalipa ushuru.