Spika wa bunge la kaunti ya Nakuru Susan Kihika anatumai kuwa bunge kuu litapitisha mswada wa theluthi mbili ya jinsia uliowasilishwa na kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale.
"Tuombe kuwa mswada huu wa theluthi mbili ya jinsia uliowasilishwa na Duale utapitishwa hii leo," aliandika kwa mtandao wa facebook.
Mswada huu ulifeli kupasishwa juma lililopita kutokana na ukosefu wa idadi ya wabunge wanaouunga mkono.
Jumla ya wabunge 233 kati ya 349 wanatakiwa kuunga mkono mswada huu ili upitishwe.