Kijana mmoja amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kupatikana na bangi.
ADVERTISEMENT
Share news tips with us here at Hivisasa
Mshukiwa, Mohamed Hussein Balala, anadaiwa kupatikana na bangi hiyo yenye thamani ya shilingi 40 mnamo Machi 21, 2016 katika eneo la Kibokoni.
Balala alikanusha madai hayo mbele ya hakimu mkuu Susan Shitub siku ya Jumanne.
Hakimu Shitub alimuachilia mshukiwa huyo kwa dhamana ya shilingi laki moja.
Kesi hiyo itasikilizwa Aprili 15, 2016.