Kijana mwenye umri wa makamo amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la wizi wa mabavu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mshtakiwa, Jamil Salim, anadaiwa kuiba simu yenye thamani ya shilingi elfu tatu, mali ya Feisal Mohamed, mnamo Mei 19 mwaka huu, akiwa amejihami kwa panga na kisu.

Bwana Salim alikanusha madai hayo siku ya Jumatatu mbele ya Hakimu Francis Kiambi.

Hakimu Kiambi aliagiza mshtakiwa huyo kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano.