Mahakama ya Mombasa imemhukumu kijana mwenye umri wa makamo kifungo cha maisha kwa kosa la wizi wa mabavu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Haya yanajiri baada ya Omar Ibrahim Otieno pamoja na wenzake wanne kutiwa mbaroni siku ya Alhamisi katika eneo la Ganjoni mjini Mombasa.

Otieno na wenzake wanadaiwa kumuibia mwanamume mmoja na mkewe waliokuwa wakielekea hospitali kumtembelea mgonjwa.

Otieno alikubali kosa hilo na kuhukumiwa kifungo cha maisha, huku wenzake wakikanusha mashtaka hayo na kutozwa dhamana ya shilingi laki tano.

Baadhi ya vitu walivyoiba ni chupa ya chai pamoja na mahamri yaliyo gharimu shilingi mia moja ,simu mbili zenye thamani ya shilingi elfu 34, pamoja na pesa taslimu.

Kesi ya washukiwa wanne waliokanusha mashtaka itatajwa Januari 3, mwakani.