Mahakama ya Mombasa imemtoza kijana mmoja faini ya shilingi elfu 50 au kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la wizi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mshtakiwa, Abdallah Salimu, amepatikana na hatia ya kuiba runinga ya Biasha Athurman, yenye thamani ya shilingi elfu nane.

Kijana huyo alitekeleza wizi huo mnamo Machi tarehe 31 katika eneo la Likoni.

Akitoa uamuzi wake siku ya Jumatano, Hakimu Susan Shitubi aliagiza Salimu kukata rufaa kabla ya siku 14 iwapo hajaridhiswa na uamuzi huo.

Mshtakiwa huyo aliitaka mahakama kupunguza faini hiyo kwa kujitetea kwa kusema hana uwezo wa kupata pesa hizo kwa kuwa familia yake inamtegemea.