Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kijana mmoja amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani, kwa kosa la kurarua nguo za mpenzi wake na kuiba simu ya rununu.

Upande wa mashtaka ulielezea Mahakama ya Mombasa siku ya Jumanne kuwa mshukiwa huyo, Billy Anyanzwa, aliingia katika chumba cha mpenzi wake Eunice Njeri, mnamo tarehe 8 mwezi wa Aprili katika eneo la Kaa Chonjo, na kurarua nguo zake zenye thamani zaidi ya shilingi elfu 30.

Mshukiwa huyo pia alichukua simu ya rununu ya mpenziwe na kutishia kumpiga.

Anyanzwa alikubali mashtaka hayo mbele ya Hakimu Diana Mochache na kuiambia mahakama kuwa alikuwa na hasira kwa vile alishuku kuwa mchumba wake alikuwa na mpenzi mwengine.

Akitoa hukumu yake, Hakimu Mochache alisema kuwa mshtakiwa amepatikana na hatia za kuharibu mali na wizi, na kumhukumu kifungo cha miezi sita kwa kila kosa.