Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama ya Mombasa imemhukumu kijana mmoja kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la wizi.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Ijumaa kuwa mshtakiwa, Saidi Juma, alipatikana na pikipiki iliyokuwa imeibiwa mnamo tarehe Agosti 28, 2015 katika eneo la Likoni, Kaunti ya Mombasa.

Hata hivyo, Hakimu Richard Odenyo alitupilia mbali shtaka la wizi wa kimbavu lililomkabili mshatkiwa huyo kwa ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

Mshtakiwa huyo alipewa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.